Skip to main content

Posts

Showing posts from July 31, 2010

SACCOS YA WALIMU

Na Friday Simbaya, Iringa CHAMA cha Ushirika cha Akiba na Kukopa cha Walimu wa Iringa Vijini na Kilolo (IRTS-SACCOS LTD) kimekabidhi pikipiki kwa walimu wanachama 19 katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya chama hicho jana. Pikipiki hizo 19, zilitolewa kwa walimu 19 kati ya 27 walikubaliwa kupewa na juhudi zaidi zinafanyika kupata pikipiki nyingine nane (8) zilizobaki ili walimu hao nao waweze kupewa mapema. Akikabidhi pikipiki kwa walimu, Afisa Elimu wa Wilaya shule za msingi (DEO), William Mkagwa, kwa niaba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa (DED), Tina Sekambo, alisema kuwa amefurahishwa na juhudi za SACCOS ya kutatua matatizo ya usafari kwa walimu wanachama kwa kutoa mikopo ya pikipiki ambazo zitarahisisha sana usafari kutokana na hali ya jiografia ya Wilaya. Aidha, Sekambo alishauri pia utaratibu wa mikopo ya vyombo hivi uwe endelevu ili hatimaye walimu wote waweze kupata vyombo hivi. “Ningependa pia nizungumza suala la mikopo, wafanyakazi wengi wame...