Idara ya Vijana ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Usharika wa Kanisa Kuu Iringa, kwa kushirikiana na huduma ya The Healing Missionaries kutoka Dar es Salaam, imeandaa mkesha mkubwa wa kusifu na kuabudu utakaofanyika Machi 20, 2026 mkoani Iringa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la kiroho linalolenga kuwakutanisha waumini na wananchi kwa pamoja katika kumsifu na kumshukuru Mungu. Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Luckson Luswema maarufu kama Kaka MC Mtumishi, amesema lengo la mkesha huo ni kumsifu Mungu na kumshukuru kwa mambo makuu aliyowatendea, huku akiwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki ibada hiyo ili kupokea baraka mbalimbali zitakazopatikana. Aidha, ameeleza kuwa mgeni mwenyeji atakuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, ambaye ataungana na viongozi wengine wa dini kuongoza ibada hiyo maalum. Kwa upande wake, Mwenye...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.