Skip to main content

Posts

Showing posts from February 6, 2017

WALIOGOMEA MAITI HOSPITALI YA AMANA KWENDA KWA WAZIRI WA AFYA

Mama wa mtoto huyo, Julieth Daudi  Na Dotto Mwaibale SAKATA la Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake kususia kuchukua mwili wa mtoto aliyejifungua kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake baada ya kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kujifungua limechua sura mpya kufuatia wazazi hao kutaka kwenda kumuona Waziri wa Afya kufikisha kilio chao. Akizungumza na Jambo Leo nyumbani kwao Dar es Salaam jana, Daudi alisema tunahitaji kwenda kumuona Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na  Watoto, Ummy Mwalimu kwa hatua zaidi kutokana na kitendo hicho walichofanyiwa na wauuguzi hao. "Mimi pamoja na ndugu zangu tutakwenda kumuona waziri ili kumpelekea malalamiko yetu" alisema Daudi. Akizungumzia mkasa huo Daudi alisema alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith  Christopher. ...

Mayrose pamoja na Baadhi ya Watanzania Waishio Marekani Katika Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa 2017

Mtaalam wa Maendeleo ya Watu Mayrose Kavura Majinge akieleza umuhimu wa Kanuni ya Dhahabu "The Golden Rule" Katika kuondoa Ufisadi na maovu mbalimbali katika jamii yetu. Fuatilia Habari kamili: maadilikitaifa.blogspot.com Profesa Nicholls Boas wa Chuo Kikuu Maryland Marekani akiwa miongoni mwa wadau Watanzania waishio Marekani akifurahia jambo wakati wa Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care, Maryland Marekani. Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa ili...

NDUGU WAGOMEA MAITI YA MTOTO HOSPITALI YA AMANA

Mzazi Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini, akiwa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na mwanahabari akidai amebadilishiwa mtoto aliyejifungua.  Mama mzazi wa Julieth, Veronica Lucas akiwa ameshika shavu kwa masikitiko kufuatia tukio hilo. Shangazi yake Julieth, Judith Christopher akielezea tukio hilo  kwa mwanahabari. Julieth Daud (kulia) akiwa na dada yake nje ya wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo. Julieth (aliyekaa kushoto), akiwa na ndugu zake nje ya  wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.  Na Dotto Mwaibale MZAZI Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake wamegoma kuchukua mwili wa mtoto kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake kutokana na kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kujifungua. Akizungumza kwa masikitiko nje ya viwanja vya hospitali hiyo Dar es Salaam jana,...

Serikali yatangaza ‘Diploma’ ndiyo kigezo cha chini cha elimu kwa waandishi wa habari

Serikali imetangaza kuwa kiwango cha chini cha taaluma anayopaswa kuwa nayo mwandishi wa habri kuwa ni 'Diploma ya Uandishi wa Habari' kwa mujibu wa kanuni za sheria mpya ya hunda za habari zilizokamilika utungaji wake hivi karibuni. Akizungumza na wana habari leo mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Nape Nnauye amesema kuwa kanuni zimeshaundwa na zimechapishwa kwenye gazeti la serikali tangu Februari 3 mwaka huu baada ya kupokea maoni ya wadau mbalimbali. "Tumesoma, tumechambua maoni ya wengi, wapo waliotaka iwe cheti, wengine diploma, wengine digrii, wapo waliotaka PhD na wapo waliotaka iwe mtu yeyote nayejua tu kusoma na kuandika. Serikali imesimama katikati ya maoni hayo. Sifa ya chini kabisa kwa kuanzia itakuwa ni diploma ya uandishi wa habari” Amesema Nape Waziri Nape amesema pia kuwa sheria hiyo imeshaanza kutumika tangu Desemba 31 mwaka 2016, ambapo yeye kama Waziri mwenye dhamana alishatoa tangazo katika gazeti la...