Skip to main content

Posts

Showing posts from April 24, 2018

Uchukuzi, Tanesco soka zakaribia nusu fainali

Mchezaji Erick Mpunga wa Uchukuzi (kulia) akijaribu kuzuia mpira unaotaka kupigwa na Kassim Mdee wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) katika mchezo wa mpira wa miguu wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. (Picha na Bahati Mollel wa TAA). IRINGA:   TIMU za soka za Uchukuzi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zilizopo kundi ‘A’ na ‘B’ zinakaribia kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mei Mosi baada ya jana kushinda michezo ya iliyofanyika kwenye uwanja wa Samora, ambapo kila mmoja zinaongoza kundi lake kwa kujikusanyia pointi sita.  Uchukuzi inafuatiwa na mabingwa watetezi Geita Gold Mine (GGM) wenye pointi mbili, NAO na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yenye pointi moja kila mmoja; wakati Tanesco inafuatiwa na Tumbaku nayo inapointi sita lakini imezidiwa magoli ya kufunga, huku RAS Iringa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa hawana pointi.  Katika mechi hizo za jana Uchukuzi wal...