MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umefanikiwa kulipa vituoni madai yanayotokana na huduma za afya kwa wakati zaidi ya bilioni 5.1 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 sawa na asilimia 148. Malipo hayo yamesaidia huduma kuboreshwa kwenye vituo mbalimbali ikiwemo watoa huduma kuhamasika na uelewa juu ya mfuko huo . Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu (Pichani )wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko huo kwa waandishi wa habari mkoani hapa. Ambapo alisema kwenye kipindi cha mwaka 2014/2015 walilipa kiasi cha zaidi ya bilioni 3.5 hali inaonyesha ongezeko kwa mwaka huu. Alisema pamoja na malipo kuongezeka lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma za afya vijijini imekuwa kikwazo sanjari na upatikanaji wa dawa vituoni. Aidha alisema lakini pia kuongezeka kwa magonjwa yakiwemo ya ukimwi ikiwemo upungufu wa watumishi katika sekta ya afya. ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.