Skip to main content

Posts

Showing posts from March 4, 2017

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA HISA ZA KAMPUNI YA TCCIA INVESTMENT

Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA, Ndibalema John Mayanja (katikati), akizungumza hii leo Jijini Mwanza kwenye mkutano na wadau mbalimbali wa biashara. Kulia ni Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, na kushoto ni Mshauri TCCIA mkoani Mwanza, Lazaro Kiheya. BMGHabari Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA, Ndibalema Mayanja, amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa ya ununuaji wa hisa za kampuni ya TCCI Investment. Mayanja ameyasema hayo Jijini Mwanza hii leo na kubainisha kwamba hisa hizo zilianza kuuzwa tangu Februari Mosi mwaka huu kwa bei ya shilingi Mia Nne na kwamba mwisho wa uuzwaji wa hisa hizo ni Machi 14 mwaka huu. "Njia pekee ya kijiendeleza kiuchumi hivi sasa ni kupitia hisa hivyo nunueni hisa hizi za kampuni ya uhakika ambayo kila mwaka huwapatia wanahisa wake gawiwo lao". Amesisitiza Mayanja na kuongeza kwamba hisa hizo zinauzwa katika benki ya ...

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA UBUNGO LAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA BILIONI MIA MOJA

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam wakiwa katika kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 (Picha zote na Nassir Bakari) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kulia kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob Kushoto ni Muweka hazina wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Jenny Machicho, Afisa utumishi Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ally Juma Ally, na Mchumi wa Halmashauri ya manispaa ya Ubungo Yamo Wambura wakiwa katika kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza wakati wa kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 (kushoto) ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe Ramadhan Kwangaya na (kulia)...

MISA TANZANIA YAWATUNUKU VYETI WANAHABARI KANDA YA ZIWA

Mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu, walionufaika na mafunzo yaliyotolewa na taasisi MISA Tanzania, akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa mwakilishi wa taasisi ya FES Tanzania (katikati), iliyofadhiri mafunzo hayo. #BMGHabari Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, imewatunuku vyeti vya ushiriki wanahabari kutoka vyombo mbalimbali katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Wanahabari waliopatiwa vyeti hivyo ni waliopatiwa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya Sheria Mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017. Mafunzo hayo ya siku mbili yalianza juzi alihamisi na kutamatika jana katika Hotel ya Adden Pallace Jijini Mwanza, yakifadhiliwa na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) tawi la Tanzania. Akizungumza mapema kabla ya kukabidhi vyeti kwa washiriki, mwakilishi wa taasisi ya FES Tanzania, Violet John, aliwahimiza wan...

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI