Skip to main content

Posts

Showing posts from March 11, 2026

RUCU Yazindua Tovuti Mpya Yenye Teknolojia Ya Akili Unde

Iringa. Chuo Kikuu cha Ruaha Catholic University (RUCU) mkoani Iringa kimezindua rasmi tovuti mpya ya kisasa iliyounganishwa na teknolojia ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI) kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa na huduma kwa wanafunzi, wazazi na wadau wa elimu. Akizindua tovuti hiyo Machi 11, 2026, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Chrispina Lekule, alisema RUCU kama taasisi ya elimu ya juu inaendelea kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani. Alisema kupitia maboresho na tafiti mbalimbali, chuo hicho kimefanikiwa kubuni tovuti ya kisasa yenye muundo unaorahisisha matumizi kwa watumiaji kupitia simu za mkononi au kompyuta. “Tovuti hii mpya (www.rucu.ac.tz) imeboreshwa kwa muundo wa kisasa unaorahisisha matumizi kwa watumiaji kupitia simu au kompyuta. Pia imeunganishwa na teknolojia inayomwezesha mtumiaji kuuliza maswali mbalimbali kuhusu RUCU na kupata majibu sahihi papo hapo,” alisema Profesa Lekule. Alifafanua kuwa teknolojia ...