Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Chira Kata ya Kenyamanyoro katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu (Remaghinga) iliyopo Mtaa wa Buguti Kata ya Rebu ambayo inayotegemewa na Wakazi Kata zote mbili za Kenyamanyori na Rebu hatika halmashauri hiyo. Zoezi hilo limefanyika leo Januari 02,2016 ambapo wananchi hao walikuwa wakifanya ukarabati wa kujaza moramu katika maeneo yaliyochimbika kutokana na maji ya mvua pamoja na kuchimba mitaro kwa ajili ya kupitisha maji wakati wa mvua. "Hii barabara ni kama imesahaulika na Halmashauri ingawaje ni mhimu sana kwani tegemeo kwa wananchi pamoja na shughuli mbalimbali kama vile ujenzi kwa kuwa hapo ng'ambo kuna shughuli za uchimbaji wa mawe hivyo malori huwa yanapita hapa kwa ajili ya kwenda kufuata mawe hayo kwa ajili ya ujenzi katika maeneo mbalimbali ya mji". Alibainisha mmoja wa wananchi hao na kuongeza kuwa imekuwa kawaida yao kufanya ukarabati wa ai...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.