Skip to main content

Posts

Showing posts from November 22, 2016

CCM ZANZIBAR YAONYANA KUHUSU UMBEA KWENYE MITANDAO YA JAMII

Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wametakiwa kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kujadili masuala yanayohusu Chama badala yake watumie vikao halali vinavyotambuliwa na Katiba ya Chama hicho. Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakati akifunga Mkutano wa Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja Kichama uliofanyika katika Shule ya Msingi Makunduchi Mkoani humo. Alifafanua kwamba tabia hiyo ya kujadili, kukosoa na kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa ngazi mbali mbali wa Chama na Jumuiya zake kupitia Mitandao ya kijamii ni utaratibu unaokwenda kinyume na miongozo ya chama hicho. Alisema Katiba ya CCM inaelekeza Kwamba mambo yote yanayogusa maslahi mapana ya Chama yajadiliwe Katika Vikao halali vinavyotambuliwa na kanuni za Chama, kwani jukwaa hilo ndiyo sehemu rasmi ya kukosoana na kupeana maelekezo. Vuai alisikitishwa na tabia hiyo na kueleza kuwa njia pekee ya...

SAKATA LA KATIBA MPYA: JUKWAA LA KATIBA WAMNG'ANG'ANIA RAIS MAGUFULI

Mratibu wa Jukwa la katiba Tanzania JUKATA Ndugu Hebron Mwakagenda Pamoja na Viongozi wengine wa mashirika yanayoshirikiana na Jukata wakionyesha Kitabu maalum ambacho kimezinduliwa Leo kwa ajili ya kuhamasisha Upatikanaji wa katiba mpya baada ya mchakato huo kukwama kusikujulikana. Kitabu hicho kinaeleza Mwelekeo wa katiba Mpya Tanzania,Tulikotoka,Tulipo,na Tuendeko (Picha na Exaud Mtei) Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) Rais Magufuli hawezi kukwepa kuhusu suala la kupatikana kwa katiba mpya kwani yeye si Rais wa mgombea huru bali amepelekwa na chama ambacho kimewaahidi watanzania kuwa katiba mpya ni miongoni mwa sera zao. Kauli hiyo ya jukwaa la katiba imekuja huku kukiwa na sintofaamu kuhusu kupatikana ama kutokupatikana kwa katiba mpya mchakato ambao ulisimama na kupisha uchaguzi mkuu mwaka 2015 na kuacha katika hatua ya Katiba Pendekezwa. Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam Mratibu wa jukwaa la katiba Tanzania Ndugu Hebron Mwakagenda...

DC HAPI AIBUA MADUDU KINONDONI,NI YALE YA TASAF

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amemuagiza Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli kumvua nyazifa za uongoni mratibu wa Mfuko wa Kusaidia kaya masikini(TASAF) katika wilaya kinondoni Onesmo Oyango baada ya kubainika kuwaingiza kwenye malipo watu 1,397 ambao hawana sifa ya kuwalipwa fedha za hizo ambao wameghalimu zaidi ya milioni 266.9. Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo... Hata hivyo,Hapi amewaomba viongozi wa Mfuko huo, ngazi ya taifa kumchukulia hatua pia mlipaji mkuu wa Taifa kwa hatua yake ya kuhusika kuwalipa watu hao, huku akijua hawana sifa ya kulipwa stahiki hizo. Pamoja na hayo,Hapi pia ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa (TAKUKURU) katika wilaya yake kufanya uchunguzi wa kina kwa wanufaika wote na TASAF ili kujilizisha kama wsanafuaika hao wanasifa za kupewa fedha hizo. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Hapi amesema baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa kwa wanufaika wote wa fedha hizo ambao...

SERIKALI YAANZA KUAJIRI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni anapenda kuwatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa kama ifuatavyo :- 1. DEREVA II – NAFASI 10. SIFA: Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II. KAZI NA MAJUKUMU: i)Kuendesha magari ya abiria na malori, ii)Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa magari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo iii)Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari, iv) Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-Book” kwa safari zote. NGAZI YA MSHAHARA - TGOS. A 2. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III - NAFASI 4 SIFA: Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na ...

MDAHALO WA MIGOGORO YA ARDHI KIJIJI CHA UGESA

Mkazi wa Kijiji cha Ugesa Kata ya Ihalimba wilayani Mufindi, mkoani Iringa akitoa maoni wakati wa mdahalo uliofanyika katika kijiji cha Ugesa wilayani humo ukilenga kutafuta suluhisho ili kupunguza migogoro ya ardhi leo.  Shirika la TAGRODE la mkoani Iringa linaendesha midahalo hiyo katika vijiji vya Ikuka, Mbigili, Mawala, Mawambala na Masalali kwa wilaya ya kilolo na vijiji vya Usokami, Ugesa, Makungu, Magunguli na Isaula wilaya ya Mufindi kupitia mradi wake wa CEGO unaohusisha jamii ya vijijini katika uwajibikaji wa masuala ya ardhi ya kijiji. (Picha na Friday Simbaya)