LUDEWA MKUU wa Wilaya ya Ludewa Bi. Georgina Bundala amepiga marufuku kwa muda usiojulikana kuchinja au kula na kusafirisha nguruwe pamoja na mazao yake kama vile nyama, mifupa, nywele na mazao ya kusindika kutokana na homa ya nguruwe kupiga hodi tena wilayani humo. Bi. Bundala alisema endapo mfanyabiashara au mfugaji yeyote atabainika akisafirisha nguruwe kutoka katika maeneo yaliyoathirika na kupeleka maeneo yasiyoathirika mtu huyo atakuwa amekiuka agizo na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Aidha amewaagiza wataalamu wote wa kilimo na mifugo, maafisa watendaji kata na vijiji kusimamia agizo hili ili kuwathibiti wale wote wasiokuwa waaminifu wanaosafirisha nyama ya nguruwe kwa siri wakidhani wanajificha. Akitoa taarifa na takwimu za ugonjwa huo kwa Mkuu wa Wilaya, Daktari wa Mifugo wilayani Ludewa Bw. Festo Mkomba alisema maambukizi mapya ya homa ya nguruwe yametokea katika tarafa ya Mwambao wa Ziwa Nyasa na sasa yapo katika tarafa ya...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.