Skip to main content

Posts

Showing posts from November 11, 2010

MAMBO YA SIASA HAYO

MWENYIKITI wa kijiji cha Nduli, Ayubu Mwenda amedai kuwa Diwani wa kata mpya ya Nduli iliyopo Manispaa ya Iringa amekuwa akimtishia kumwondoa madarakani na pia kumnyang’anya ardhi na kuikabidhi kwa serikali ya kijiji kutokana na chuki za kisiasa. Chuki zilizotokana na wote kuomba kuteuliwa katika kura za maoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya Udiwani kwenye kata hiyo ambapo mwenyekiti huyo hakubahatika kupata nafasi na kukata rufaa ya kupinga matokeo ya kura za maoni lakini rufaa yake ilikataliwa na Idd Chonanga kupita kuwania udiwani. Mwenda amedai kuwa vitisho hivyo alianza kuvitoa mara baada ya kupita kwenye kura za maoni pamoja na kwenye kampeni ya kujinadi kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu (Oktoba 31, 2010). “Pamoja na kuwa kampeni meneja wa CCM wa kata ya Nduli lakini nimeonekana kuwa mpinzani kwake kwani alihisi kutokana na kushindwa kwangu ningesaidia vyama vya upinzani dhana ambayo si kweli kwa kuwa mimi ni kada wa CCM” alisema Mwenda. Alisem...

TANGA BATHING CLUB BEACH

Mzee Rashid Abubakari Mokiwa (Kulia) akibadilishana mawazo na mmiliki wa blog hii Bw. Friday Simbaya alipotembelea 'Tanga bathing Club' jijini Tanga leo, huku 'Kisiwa cha Tanga' kikionekana kwa mbaaaali katika Bahari ya Hindi. Mzee Mokiwa ni moja ya wahudumu wa club hiyo kwa muda mrefu sana na mwenye historia nzuri ya mahala hapa tangu enzi za wajerumani hadi leo. Ijulikane kuwa wazee kama hawa ni hazina kubwa kwa taifa letu. 'Kitunze kidumu'

MARALIA INAKUBALIKI KWA MTINDO HUU?!

Matumizi mabaya   ya vyandarua haya hapa, badala ya kutundikwa Vitandani ili kujikinga na mbuu sasa vyatumika kuvulia dagaa na samaki, kama watoto wadogo alivyokutwa wa kitumia chandarua cha 'Malaria Hakubaliki' wakivulia samaki katika bahari ya Hindi maeneo ya 'Tanga bathing Club Beach' karibu na Kisiwa cha Tanga jijini Tanga mchana leo. (PICHA. FRIDAY SIMBAYA)

CHAVITA YAOMBA SERIKALI KUBORESHA MAISHA YA WALEMAVU

CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Iringa chaiomba serikali kuboresha mazingira na maisha ya watu wenye ulemavu nchini za kupata huduma za elimu, afya na usalama wa raia kama watu wengine. Mwenyekiti wa CHAVITA Mkoa wa Iringa Zawadi Sumani alisema jana katika warsha ya ushawishi na utetezi kwa watendaji wa idara za serikali na viongozi wa serikali za mitaa Mkoa wa Iringa, kuwa watu wenye ulemavu ni waathirika wakubwa wa umaskini na UKIMWI hapa nchini kutokana na mitazamo potofu ya jamii inayoizunguka. Alisema kuwa huduma na sheria mbalimbalinzilizopo hapa nchini hazikidhi maitaji ya watu wenye ulemavu na wemekuwa wakiacwa nyuma katika mchakato mzima wa maendeleo ya taifa ingawa zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata huduma za elimu, afya na usalama wa raia. Lakini bado inaelekeza dhana kuwa mtu mwenye ulemavu anastahili kuishi maisha tegemezi ambapo dhana hii ina kwenda kinyume na tamko la u...