Skip to main content

Posts

Showing posts from February 18, 2026

Aomba Kuteuliwa Ubunge, Amuomba Samia Suluhu Hassan Amkumbuke

Iringa. Mwenyekiti wa Wazazi Wenye Watoto Wenye Ulemavu Mkoa wa Iringa, Bw. Zawadi Msigalla, amesema ana ndoto ya siku moja kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwatetea watu wenye ulemavu na makundi maalum, akimuomba Rais Samia Suluhu Hassan amkumbuke katika nafasi 10 za uteuzi wa wabunge. Bw. Msigalla, ambaye ni mtu mwenye ulemavu, amesema dhamira yake ya kuingia bungeni inatokana na uzoefu wake wa muda mrefu katika utetezi wa haki za watoto wenye ulemavu na wazazi wao, akibainisha kuwa sauti ya kundi hilo bado haijapewa uzito unaostahili katika vyombo vya maamuzi. “Nina ndoto ya kuwa Mbunge ili niweze kuzungumza kwa niaba ya wazazi na watoto wenye ulemavu. Tuna changamoto nyingi zinazohitaji uwakilishi wa moja kwa moja,” amesema Msigalla. Akizungumza na Pamlomo- Sauti Ya Jamii mesema anaamini kuwa kupitia nafasi za uteuzi wa Rais, bado kuna fursa kwa watu wenye ulemavu na watetezi wao kushiriki kikamilifu katika kutunga na kusimamia sheria. Mbali na kuwa mwenyekiti w...