Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza akimemshukuru Zakaria Hanspope kwa moyo wake wa kurudisha fadhila nyumbani na kuwaomba wananchi kushirikiana na jeshi hilo kufanikisha utendaji wake juzi. Anayeshuhudia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye (kulia). (Picha na Friday Simbaya) IRINGA: Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye ameziomba Halmashauri za Manispaa, na majiji nchini kutoa kipaumbele cha visima vya kuchota maji ya zimamoto wakati wa ujenzi wa barabara kwenye maeneo yao. Andengenye ameeleza hayo juzi kwenye hafla ya makabidhiano ya gari jipya la zima moto lenye uwezo wa kujaza lita elfu tano ambalo limetolewa na mfadhili kwa lengo la kutatua changamoto ya gari inayoukabili mkoa wa Iringa. Kauli ya Kamishana Jenerali wa Jeshi la Zimamoto inatokana na ukweli kuwa miji mingi na majiji ina msongamano wa nyumba huku kukiwa na visima vichache vya kukinga maji wakati...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.