IRINGA: Kaimu Balozi wa Marekani Dk Inmi Patterson amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kushughulikia masuala ya udamavu na utapiamlo vinavyoathari wananchi wengi nchini . Balozi huyo alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa ghala jipya la Mama Seki sambamba na mashine ya kusaga unga wa mahindi wa lishe bora iliyotolewa kwa msaada wa serikali ya marekani kupitia mradi wa NAFAKA, ikiwa sehemu ya ziara yako mkoani Iringa. Dk Patterson alisema kuwa Tanzania ina aslimia 34 ya wakazi wake wanaoishi na udumavu na utapiamlo huku wilaya za Iringa, Njombe na Songwe zote zikiwa na viwango vya utapiamlo kwa zaidi ya asilimia 40. Alisema kuwa juhudi zaidi zinahitajika katika kuboresha masuala ya elimu bora na lishe bora ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali ya kupunguza matatizo ya udumavu na utapiamlo nchini. Alisema kuwa ukosefu wa lishe unamfanya mtu asiweze kufikia malengo yake kwa vile udumavu huath...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.