HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa imetoa mkopo kwa vikundi 35 vya wanawake na vijana ikiwa ni utekeleza wa agizo la serikali la kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi hivyo jana. Akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 70,000,000/- kwa vikundi hivyo katika awamu ya pili ya kipindi cha mwaka 2016/2017, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Alex Kimbe amewataka kinamama na vijana kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili ziweze kuleta manufaa na kuwatoa katika lindi la umasikini. Alisema kuwa jumla ya vikundi 35 toka katika kata zote 18 za Manispaa ya Iringa vimepokea mikopo, ambapo vikundi 16 vya vijana vimepokea jumla ya shilingi milioni 32,000,000/- na shilingi milioni 38,000,000/- zimetolewa kwa vikundi 19 vya wanawake. Kimbe alisema mkopo huo umetolewa kwa awamu ya pili, ambapo kwa awamu ya kwanza kipindi cha mwaka 2016/2017 Halmashauri ya Manispaa ya Iringa i...