Otilinda Mambi (38), mkazi wa Kijiji cha Milongi Kata ya Lusewa Wilayani Namtumbo, ni mmoja wa wazazi saba waliojifungua siku ya mkesha wa Mwaka Mpya katika Hospitali ya St. Joseph Mission Hospital Peramiho, Mkoani Ruvuma. Watoto saba waliyozaliwa siku ya mkesha wa Mwaka Mpya katika Hospitali ya Misheni ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho mkoani Ruvuma, wakiwemo wakike wanne na wakiume watatu ni pamoja na mama mwenye umri wa miaka 38 ambaye ameishi katika ndoa zaidi miaka 20. Mambi aliolewa tangu mwaka 1990 na mume wake Winfred Ngonyani katika Kijiji cha Milongi kata ya Lusewa wilayani Namtumbo lakini hawakubahati ka kupata mtoto hata mmoja, hali ambayo ilipelekea majirani kuwanyoshea vidole kuwa ni watu wasio zaa. Lakini kabla sijaendelea na kisa hiki, hebu tuangalie tafsiri ya maana ya ndoa ni nini? Ndoa ni chombo cha mume na mke chakufanya kazi za ustawi wa ujamii na uimarishaji wa familia. Kudumu kwa ndoa hutegemea jinsi mume na mke wanavyokiendesha na kukitunza c...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.