Iringa. Jamii ya Wahaya wanaoishi Manispaa ya Iringa imefanya sherehe maalumu ya kuuaga mwaka 2025 na kuukaribisha mwaka 2026 kwa shamrashamra kubwa, katika hafla iliyopewa jina la “Abanywani” likimaanisha marafiki. Sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Iringa iliwakutanisha Wahaya kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo wakiwemo familia, vijana na wazee, kwa lengo la kuimarisha mshikamano, kuendeleza utamaduni wao na kusherehekea mafanikio ya mwaka uliopita. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, mmoja wa waandaaji Kaijage Rwezaula alisema neno Abanywani linaakisi urafiki, upendo na umoja miongoni mwa wanajamii, huku likiwaalika pia watu wa makabila mengine kushiriki na kujifunza utamaduni wa Kihaya. “Tumekutana hapa si tu kwa ajili ya burudani, bali kuimarisha undugu wetu na kusaidiana kama marafiki na ndugu tunaoishi mbali na nyumbani,” alisema Kaijage Katika sherehe hiyo, washiriki walipata fursa ya kufurahia vyakula vya asili ya Kihaya, muziki wa asili pamoja na bur...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.