Skip to main content

Posts

Showing posts from May 17, 2011

SEMINA KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU TZ

Katibu wa CWT Mkoa wa Ruvuma ambaye pia alikuwa ndiye Mratibu wa Mafunzo, Mwl. Luya Ngonyani akitoa mada wakati ya semina ya sera ya mafunzo na haki kwa viongozi wa CWT kutoka Kata Nne za Litisha, Maposeni, Peramiho na Lilambo wilayani Songea. Jumla ya washiriki wa semina hiyo ni 40. Semina hiyo ilifanyika leo Peramiho Shule ya Msingi, Songea Vijijini. Washiriki wa semina ya sera ya mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi CWT na wawezeshaji muda mfupi baada ya kumalizika kwa semina hiyo. walioketi kutoka kushoto kwenda kulia ni Mwl. Mwahija Luambano Mwakilishi wa Walimu Wanawake wilayani Songea, Mwl. Gervas Ngondo Mweka Hazina CWT, Mwl. Luya Ngonyani Katibu CWT Mkoa/ Mratibu wa Mafunzo, Mwl. Beno Mwenda Mwenyekiti CWT Wilaya na Mwl. Manyula M. Nkomolla Katibu CWT Songea Vijijini.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KATIKA KUMSIMIKA ASKOFU NDIMBO

ASKOFU MTEULE WA JIMBO LA MBINGA MHASHAMU JOHN C. NDIMBO RAIS Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kumsimika Askofu Mpya wa Pili wa Jimbo Katoliki la Mbinga mkoani Ruvuma hapo tarehe 05.06.2011. Aidha, Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu huyo itaongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Da es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. Akiongea na Blog ya http://www.fridaysimbaya.blogspot.com/ leo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Jimbo la Mbinga Pd. Jospeh Mwingira amesema kuwa Rais Kikwete ndiye atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kumsimika rasmi na kuweka wakfu Askofu Mteule wa Jimbo la Mbinga, Mhashamu John Chrisostom Ndimbo. Jimbo Katoliki la Mbinga limepata Askofu Mpya aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Pili wa Jimbo hilo. Mwashamu Askofu John Ndimbo aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Askofu wa pili wa Jimbo Katoliki la Mbinga hapo tarehe 12 Machi, 2011. Uteuzi huo umefuatia kustaafu kisheria kwa Mhasha...