Skip to main content

Posts

Showing posts from September 27, 2017

YALIYOJIRI KIAKO CHA BARAZA LA BIASHARA LA MKOA WA IRINGA

Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Iringa Amina Masenza, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoawa Iringa akitoa hotuba akionja majani ya stevia yenye sukari nyingi huku Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu akishuhudia wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana. ####################################### Masenza alitoa rai kwa wajumbe na wadau mbalimbali kutumia fursa vizuri zilizopo mkoani iringa kutengeza ajira kwa wananchi husani vijana. Aidha, ajira hizo zitakuza pato la mwananchi mmoja mmoja kwa kwa taifa nzima. Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akitoa maoni wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) mkoa wa Iringa Odilo Ngamilaga akitoa maoni wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Valentine mjini Iringa jana. Kushoto...

TANAPA: INAKUPELEKA KUTALII HIFADHI YA RUAHA KWA 30,000/- TU KWENDA NA KURUDI

IRINGA: Wananchi wa mikoa ya nyanda za juu kusini wameaswa kutumia fursa ya siku mbili maonesho ya utalii karibu kusini kuitembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha iliyopo wilayani Iringa, mkoani Iringa. Akizungumza na waandishi wa habari ya meneja masoko wa shirika la hifadhi za Tanzania (TANAPA) aliwaomba wananchi kutumia siku mbili za maonesho ya utalii yanayofanyika kwa wiki moja mjini iringa kwenda hifadhi ya ruaha kwa gharama nafuu. Alisema kuwa TANAPA kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini inatenga siku mbili maalumu kwa ajili wananchi kwa ajili ya wananchi kutembelea hifadhi hiyo kwa gharama nafuu katika ya septemba 28 -30 mwaka huu. “Kwa kupitia ofa hiyo kutakuwa na mchango mdogo wa fedha; mtu mzima atalazimika kuchangia Sh 30,000 na mtoto Sh 10,000 tu kumuwezesha kwenda kwa siku moja kutalii katika hifadhi hiyo kubwa kuliko zote nchini,” alisema. Alisema mchango huo unahusisha gharama ya usafiri, kiingilio cha hifadhini, utalii na muongoza wageni ata...