Skip to main content

Posts

Showing posts from August 1, 2016

MKUTANO WA LOWASSA NA WANAFUNZI MUHIMBILI WAZUILIWA

Na Dotto Mwaibale UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia mkutano uliokuwa ufanywe na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowaasa. Mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike na baadhi ya vijana wa kikristo ambao ni wanafunzi wa chuo hicho ulikuwa pangwa kufanyika juzi chuoni hapo kuanzia saa za mchana. Akizungumza mtandao wa www. habari za jamii.com mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema maandalizi yote ya mkutano huo ambao ulikuwa baada ya ibada yalikuwa yamekamilika. "Tulifanya taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo ambao ulitukubalia na kumualika ndugu Lowassa lakini tumeshangazwa na zuio lililotolewa na uongozi wa chuo" alisema mwanafunzi huyo. Mwanafunzi huyo alisema kuwa saa sita mchana wakati wakimsubiri mgeni rasmi Edward Lowassa awasili mkuu wa chuo hicho na viongozi wengine waliwaita na kuwaeleza kwamba mkutano huo umewekewa zuio kutoka juu hivyo ha...

DC MTATURU ATENGA SIKU YA JUMAPILI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akielekezwa jambo na muwekezaji wa miche ya miti Wikayani humo Mr Choi Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakikagua ujenzi wa matundu ya choo Na Mathias Canal, Singida Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu Leo amekagua miradi ya maendeleo katika kijiji cha Utaho A ambapo inajengwa shule mpya ili kupunguza adha ya watoto kwenda umbali mrefu na kuvuka barabara ambapo pamoja na kupatiwa mafunzo ya usalama barabarani lakini bado ni Hatari kwao. Mtaturu amewapongeza wananchi kwa kazi nzuri wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki kingu na Diwani wa Kata ya Kituntu kusimamia vyema shughuli za maendeleo na hatimaye kufanikiwa kupaua madarasa mawili na ofisi ya walimu. Sawia na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza viongozi wote katik...