Skip to main content

Posts

Showing posts from February 14, 2018

Mama Samia aahidi kupunguza msongamano hospitali ya Mafinga

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imeanza kupanua vituo vya afya nchini pamoja na kuboresha huduma za matibabu ili kupunguza msongamano wa watu katika hospitali za wilaya.  Mama Samia alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipotembelea na kuweka jiwe la msingi na kukagua maendeleo ya upanuzi wa Kituo cha Afya Ihongole katika Kijiji cha Ihongole nje kidogo ya Mji wa Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa.  Alisema kuwa Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika boresha utoaji wa huduma afya katika vituo vya afya katika wilaya ili kupunguza msongamano mkubwa uliopo kwenye hospitali za wilaya pamoja nza mikoa.  “Tukishapunguza msongamano madaktari wetu watafanya kazi kwa uhakika zaidi na kwa umakini mkubwa,” aliongeza makamu wa rais.  Hata hivyo, makamu wa rais halmashauri ya mji wa mafinga, wilayani Mufindi kwa kutumia fedha vizuri zilizotoalewa na serikali kwa ajili ya shughuli za upanuzi wa kituo cha Ihongole....