Skip to main content

Posts

Showing posts from February 20, 2014

TUPSE: WAAJIRI NCHINI WANATAKIWA KULIPA MAPUNJO YA MISHAHARA KWA WAFANAYAKAZI

Na Friday Simbaya, Songea Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Walinzi Binafsi Tanzania (TUPSE) Taifa , Edson  Eliya Kivelege amewataka waajiri  nchini kuwalipa wafanyakazi mapunjo  ya mishahara  yanayotokana  kupandishwa kwa kima cha chini cha mishahara na serikali mwaka jana kabla  ya sheria haijakuchua mkondo wake. Alisema mapunjo hayo yanatokana  na waajiri wengi wa makampuni ya walinzi  binafasi kutolipa viwango vipya vya mishahara baada ya serikali  kupitia bodi ya mishahara kutangaza kima cha chini kwa sekta zote mwezi wa saba mwaka 2013. Katibu huyo wa TUPSE alisema hayo wakati wa  mahojiano maalum  na NIPASHE  alipofanya ziara yake katika Nyanda za Juu Kusini kwa lengo kukagua uhai wa chama  pamoja na kufanya maandalizi  ya  kufanyika kwa mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika hivi karibuni  jijini Dar es Salaam. Aidha, Kivelege  alimteua  Zacharia Godwin Mfilinge kuwa mwakilis...