Na Friday Simbaya, Peramiho Ijumaa ya tarehe 19 Novemba ya mwaka 2010 Chuo cha Ufundi cha Peramiho (Peramiho Vocational Training Center) kilichopo Jimbo la Songea, mkoani Ruvuma, kilifanya mahafali yake ya 79 ambapo jumla ya wahitimu 23 walitunikiwa vyeti vya kumaliza mafunzo katika fani mbalimbali. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 23 walitunukiwa vyeti vya kumaliza mafunzo katika fani ya ushonaji, ufundi magari na useremala ambapo vijana waliohitimu wanakamilisha idadi ya wahitimu jumla 1,718 katika chuo hiki tangu kuanzishwa kwake mwaka 1928. Chuo cha ufundi Peramiho kilipata usajili kwa mujibu wa sheria za nchi kwa kuendasha mafunzo chini ya uratibu na muongozo wa VETA ambao ni waratibu wakuu wa mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania. Mahafali hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Mtakatifu Benediktini hapa Peramiho na kuhudhulia na wageni mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali za hapa Peramiho (Shule ya Wasichana Peramiho, Sekondari ya Sili, Sekondari Maposeni, Daraja...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.