Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya miundombinu ya barabara mkoani Mbeya, ikiwemo ujenzi wa barabara ya njia nne (dual carriageway) yenye urefu wa kilomita 29 kutoka Uyole (Nsalaga) hadi Ifisi, pamoja na upanuzi wa barabara ya mchepuo katika eneo la Mlima Nyoka lililopo kwenye barabara kuu ya TANZAM. Mradi wa barabara ya njia nne Uyole–Ifisi unatekelezwa na Mkandarasi M/s China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO), huku Mhandisi Mshauri akiwa ni TECU, kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 138 bila kujumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Akizungumza na Pamlomo24 Updates, Mkuu wa Kitengo cha Miradi ya Maendeleo katika Ofisi ya Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Justin Mrope, kwa niaba ya Meneja wa TANROADS Mkoa huo, Mhandisi Suleiman Bishanga, alisema mradi huo ni sehemu ya uboreshaji wa barabara kuu ya TANZAM. Alisema katika utekelezaji wa mradi huo, jumla ya wananchi 117 kutoka kata za Iyunga, Iwambi na Nsalala jijini Mbeya wame...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.