Skip to main content

Posts

Showing posts from July 31, 2017

MAADHIMISHO YA 88 KITAIFA KUFANYIKA LINDI KUANZIA KESHO

Maonesho ya Kilimo (NaneNane) yanataraji kuanza kesho Agosti 1, 2017 kote nchini kwa ngazi mbalimbali za kanda huku Maonesho hayo Kitaifa yakifanyika Mkoani Lindi huku Maandalizi na maonesho ya Ki-Kanda yanaratibiwa na uongozi wa mikoa husika. Maandalizi ya Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane yatafanyika kwa siku 8 ambapo Kitaifa yatafika ukomo jioni ya Agosti 8, 2017 katika Viwanja vya Ngongo na Maeneo mengine yatakapoadhimishwa kikanda katika viwanja vya maonesho ni John Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere –Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni - Dodoma; Nyahongolo – Mwanza; na Fatuma Mwassa - Tabora.  Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo hutoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini.  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg Mathew Mtigumwe wakati akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru....

MWIGULU AKEMEA SIASA ZA KISHAMBA NCHINI

Na Friday Simbaya, Iringa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amesema Tanzania bado kuna ulimbukeni wa demokrasia kwa kubaguana katika misingi ya vyama vya siasa. Mwigulu alitoa kauli hiyo jana (JUMAPILI) wakati akitoa salamu za serikali katika ibada maalum ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Mlandege katika Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa.  Alisema kuwa bado anashangaa kuona watu wanabaguana kwa itikadi ya vyama pamoja na siasa ya vyama vingi nchini kudumu kwa miaka zaidi ya 20 sasa. “Inatakiwa watu tuwe tunataniana kama tunavyotaniana kwenye mpira na ndugu yangu DC Kasesela kuhusu Singida united na Lipuli FC au mpira wa Yanga na Simba…,” alisema Mwigulu. Mwigulu aliambatana na mwenyeji wake Richard Kasesela ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa. Aidha, ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Iringa Blaston Tuluwene Gaville akisaidiana na mchungaji kiongozi Rhod...

UWANJA WA SONGWE CHUPU CHUPU UTEKETEE

Taharuki imewakumba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (Sia) mkoani Mbeya na wananchi wanaofanya shughuli kando mwa barabara kuu ya Tanzania -Zambia baada ya moto kuwaka ndani ya eneo la uwanja huo. Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika ulitokea jana mchana na kaimu meneja wa uwanja huo, Jordan Mchami alisema iliwachukua takriban nusu saa kuuzima. Alisema moto huo ulianzia katika eneo la barabara kuu ya Tanzania - Zambia umbali wa mita 600 kutoka maeneo yalipo majengo na eneo la kurukia ndege. “Tumefanikiwa kuuzima, hakuna madhara yoyote katika eneo letu na si sahihi kusema uwanja umeungua. Ifahamike kwamba uwanja huu una eneo kubwa ambalo ni kama vile pori tu. Moto umetokea barabara kuu ya Tanzania -Zambia umbali wa mita 600 hivi hadi tulipo sisi,” alisema baada ya kuenea taarifa katika mitandao ya kijamii na maeneo ya jirani kwamba uwanja huo umewaka moto. Alipoulizwa kuhusu cha moto huo Mchami alisema ulionekana kuanzia barabarani na walipofuatilia kwa kuw...