Skip to main content

Posts

Showing posts from October 4, 2010

HABARI KATIKA PICHA

  Gari la tumbukia darajani karibuni na Kijiji cha Kidamali huko meneo ya Kalenga wilayani Iringa hivi karibuni lakini hakuna mtu waliyepoteza maisha kutokana na ajali hiyo. Imeelezwa kuwa dereva wa gari hiyo alikuwa amelewa pombe ndipo gari lilimshinda kutokana na mwendo kasi.  Mgombea udiwani Kata ya Rujewa wilayani Mbarali kupitia tiketi ya NCCR-Mageuzi, Bw. Abubakari Said Chomba akihutubia wananchi wa Kata ya Rujewa katika mkutano wake wa kampeni katika uwanja wa Mzee Mlidi katani humo hivi karibuni.   Wanahabari walipo kuwa ofisi ya NAFCO inayotumiwa na muwekezaji katika mashamba ya Mbarali ya Mpunga kutoka kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania mkoani Iringa Bi. Oliver Richard Motto, Bw. Sufiani Muhidini Mpigapicha wa gazeti la Mtanzania na mwandshi wa kujitegemea na mmiliki wa blog hii Bw. Friday Simbaya wakiwa katika picha ya pamoja.  Mkazi wa Rujewa Wilaya Mbarali ambaye hakufahamika jina lake mara moja akiokota makopo katika jalajala...