Skip to main content

Posts

Showing posts from September 22, 2015

UN NA SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI ILIYOPO NCHINI

Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nyanza jijini Mwanza kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani ambapo kitaifa yamefanyika jijini humo na kuandaliwa na Baraza la Dini mbalimbali la Amani Tanzania (IRCPT) kwa ushirikiano wa UNESCO ambapo yaliwashirikisha Viongozi wa Serikali, Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Viongozi wa madhehebu ya dini, Jeshi la Polisi, Walemavu, Wananchi pamoja na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na wa pili kulia ni Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog ). Na Mwandishi Wetu, Mwanza Um...