Skip to main content

Posts

Showing posts from July 18, 2011

MHANDISI AKESHA ENEO LA MRADI WA MAJI

MHANDISI  WA MAJI LUDEWA ASHANGAZA KWA KUACHA FAMILIA NA KUKESHA ENEO LA MRADI KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA MAJI SALAMA NA KWA WAKATI.            WANANCHI katika Kata za Manda, Luilo na Masasi katika Tarafa ya Masasi Ludewa, mkoani Iringa wameiomba serikali kuongeza nguvu zaidi katika mradi wa maji uliokuwa umeshindikana muda mrefu ama kwa kukosa rasilimali wataalamu wenye uwezo au fedha ili kuweza kufikisha maji katika maeneo yaliyobaki baada ya Bw. Christopher Nyandiga (Mhandisi wa Maji wilayani humo) kufauru kufikisha maji katika baadhi ya maeneo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau, wananchi na watumiaji wa maji hayo hawakusita kumshukuru na kumpongeza mhandisi wa maji wilayani humo Bw. Christopher Nyandiga na kumtaja kama mkombozi wa maisha yao kwa kuwa ni miaka mingi maji ya bomba yamekuwa ndoto kwao kutokana na ukilitimba wa wataalam na wahandisi waliotangulia. “Mradi wa maji katika Tarafa yetu ya Masasi una historia ya ...

VIBALI VYA MADINI LUDEWA

LUDEWA WANANCHI Wilayan ya Ludewa mkoani Iringa wako hatarini kugeuka wakimbizi katika siku za usoni kutokana na hofu ya maeneo yao kugawiwa kinyemela na ofisi za madini kanda zilizoko mkoani Mbeya imefahamika. Hofu na mashaka vilitanda hivi karibuni kwa madiwani wote walipotembelea katika Kata ya Iwela ambako kulikuwa na wasiwasi miongoni mwa wananchi waishio katika maeneo hayokuwa baadhi ya wachimbaji wageni wenye mitambo wasio na vibali wameingia na kuvamia kwa kuanza shughuli za uchimbaji bila wananchi kujulishwa. Katika Baraza la Madiwani (Full Council) madiwani katika halmashauri hiyo waliitaka Wizara ya Nishati na Madini kutumia busara na uungwana kuhusu suala la ugawaji maeneo kwa sababu pamoja na kuwepo Sheria za Madini,  lakini wananchi nao wanayo haki ya kusikilizwa na kuhusishwa ili kuepusha migongano ya baadaye. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Matei Felician Kongo akizungumza katika baraza hilo alioneshwa kusikitishwa kwake kusikia kila eneo ndan...

LUDEWA WAGOMA KUWAPOKEA WATANZANIA WAPYA

WANANCHI katika Wilaya ya Ludewa Mkoani Iringa, wamekataa katu kuwapokea wakimbizi kutoka Somalia na Ethiopia waliobatizwa kwa jina la watanzania wapya kwa madai kuwa watasababisha hasara kubwa kuliko faida imefahamika. Mgomo huo umetokea jana katika kikao cha Baraza  la Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi kilichofanyika Julai 15 mwaka huu ambacho pamoja na mambo mengine kilihusisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa miradi  ya maendeleo kwa mwaka wa fedha uliopita. Awali akitoa taarifa ya kutaka ufafanuzi Diwani wa Kata ya Mawengi, Bw. Leodgar Mpambalyoto alisema kuna jambo lililoko mbele yetu linalowasumbua wananchi wengi ambalo ni agizo la serikali la kuwapokea watanzania wapya ambao wamebatizwa jina hilo kutokana na kuingia nchini na kupokelewa kama wakimbizi. Kwa upande, wake Mpambalyoto aliishauri serikali kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi na baadhi ya wadau wakiwemo madiwani. “Ni wajibu wa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa ...

WANANCHI LUDEWA WAPIGANA VIKUMBO NA MIFUGO KISA MAJI

Na Friday Simbaya, Ludewa WANANCHI wa Ludewa Mjini Makao Makuu ya Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa wamesema kuwa hawaoni umuhimu wa kuwa na mamlaka ya maji mjini yaani ‘Ludewa Water Supply and Sanitation Authority (LUDSSA) kwa sababu tatizo la maji kwao linazidikuongeka kila kukicha huku mabomba yakitiririsha maji mitaani ovyo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema Serikali ya Wilaya ya Ludewa haioni haja ya kusumbua vichwa kwa ajili ya kuondoa kero ya maji kwa sababu katika nyumba zao maji yamejaa mpaka wanashindwa kwa kuyapeleka kwani mwenye shibe hamjali mwenye njaa. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ludewa mjini, Bw Omary John Kiowi alisema kuwa wananchi wanayo haki ya kulalamika kwani kero hii ni aibu kwa wataalam wetu ambao miaka nenda rudi wanatoa sababu kuwa maji hayatoshi kwenye matanki huku waamebweteka bila kutafuta njia mbadala kuikabili hali hiyo. Bw Benito Mgimba makazi wa Mtaa wa Kanisa B aliliambia Nipashe kuwa sasa ni miaka zaidi ya kumi maji katika m...