Skip to main content

Posts

Showing posts from February 7, 2018

MKUU WA WILAYA AWAAMURU MADEREVA KUSHUSHA MBOLEA

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Luckness Amlima Leo ameamuru mbolea iliyokuwa imeletwa wilayani humo kwa ajili ya wakulima wa zao la Tumbaku na madereva kuzuia kushusha mbolea hiyo wakidai walipwe gharama za usafirishaji wa mbolea hizo ameamuru zishushwe mara moja na wagawiwe wakulima. Akiongea na madereva na wakulima hao katika viwanja vya ushirika wilayani humo mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa hakuna sababu ya kuendelea kubaki na mbolea kwenye magari huku wakulima wakilalamikia tumbaku inaharibika kwa kukosa mbolea. “Shusheni mbolea kwani madai ya fedha ya kusafirishia mbolea hiyo yanafanyiwa kazi na chama kikuu cha Ushirika SONAMCU alisema mkuu wa wilaya huyo. Aidha mwandishi msaidizi wa chama cha msingi Namtumbo bwana Nasoro Makomaye alisema kuwa mbolea ilifika wiki mbili zilizopita lakini madereva walikataa kushusha mbolea hiyo wakidai fedha ya kusafirishia mbolea hiyo. Bwana Nasoro alimshukuru mkuu wa wilaya ya Namtumbo kwa kuwasi...

MEYA MANISPAA YA IRINGA ABADILISHIWA HATI YA MASHITAKA

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Iringa imeahirisha kesi inayomkabili Meya wa Maanispaa ya Iringa Alex Kimbe ya kutishia kuua mtu kwa bastola hadi kesho baada ya mwendesha mashitaka wa upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya mashitaka ya kesi hiyo.  Kesi hiyo namba 189 ya mwaka 2017,ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa hoja za awali na upande wa Jamuhuri ulidai uko tayari lakini wakili wa upande wa utetezi Samson Rutebuka alidai mahakamani hapo kuwa hakuwa tayari kwa hatua hiyo kutokana na kuhitaji muda kwa ajili ya kujisoma kabla ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo. Hakimu Mpitanjia alihoji upande wa Jamuhuri sababu za wakili wa utetezi kutopatiwa hati hiyo hadi jana ambapo alijibiwa kuwa ni kutokana na dhamira ya Jamhuri kutaka kubadilisha hati ya Mashitaka. "Mheshimiwa Hakimu tumeshindwa kumpatia wakili wa utetezi hati ya mashitaka kwa kuwa tunatarajia kuwasilisha ombi la kubadilisha hati hiyo ,hivyo tusingempatia kabla haijasajiliwa mahakamani,'alisem...

MADIWANI WANNE WAPYA WAPISHWA MANISPAA YA IRINGA

Diwani wa Kata ya Kitwiru (kushoto)kupitia CCM anakula kiapo mbele ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Iringa katika Jimbo la Iringa Mjini huku hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa David Ngunyale (kulia) akisimamia kiapo hicho jana. (Picha na Friday Simbaya) Diwani wa Viti Maalum Rehema Mbetwa (kushoto) anakula kiapo mbele ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Iringa huku hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa David Ngunyale (kulia) akisimamia kiapo hicho jana. (Picha na Friday Simbaya) MADIWANI wanne wapya wa Manispaa ya Iringa wawili kutoka CCM na wawili kutoka Chadema wameapishwa leo na kukabidhiwa nyaraka mbalimbali tayari kwa kuanza kazi ya uwakilishi wa wananchi katika maeneo yao jana.  Walioapishwa katika baraza la madiwani ya robo ya pili ya mwaka 2018 ni pamoja na Jully Sawani kupitia CCM kata ya Kihesa ambaye katika uchaguzi wa Janauri 13 alipita bila kupingwa baada ya vyama vya upinzani kususia...