Skip to main content

Posts

Showing posts from July 25, 2015

Maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa Mkoani Iringa

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Iringa Mhe. Amina J Masenza (kuume) na Mshauri wa Mgambo Mkoa Meja Akili katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa Mkoani Iringa.

Hepautwa:nafahamu maumivu yaliyotokea kwa wana CCM baada ya kuichagua Chadema uchaguzi wa mwaka 2010

Nuru Hepautwa Na Friday Simbaya, Iringa KADA maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mjini Iringa, Nuru Hepautwa amesema anafahamu maumivu yaliyotokea kwa wana CCM baada ya kuachia jimbo hilo mikononi mwa Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2010 lakini akaahidi kuyamaliza endapo atapewa ridhaa hiyo. Hepautwa ambaye pia ni mfadhili wa mashindano ya soka yaliyojizolea umaarufu mjini Iringa ya Hepautwa Cup alitoa mchango huo jana wakati akijinadi kwa wanachama katika Kata ya Kitwiru Jimbo la Iringa mjini. MFANYABIASHARA huyo alitangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa Mjini hivi karibuni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwa kupitia tiketi ya chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM). Hepautwa ambaye pia ni Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Iringa Mjini alisema anafahamu maumivu yaliyotokea kwa wana CCM baada ya kuachia jimbo hilo mikononi mwa Chadema katika uchaguzi lakini akaahidi kuyamaliza endapo ...

UWT CCM MKOA WA IRINGA WACHAGUANA

Rose Tweve Ritta Kabati Lediana Mng'ong'o wajumbe Zainabu Mwamwindi wagombea UMOJA wa Wanawake wa Tanzania (UWT) mkoa wa Iringa umekataa kumuongezea kipindi kingine cha miaka mitano bungeni, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Lediana Mng’ong’o (58) katika mkutano wake wa kura za maoni uliofanyika juzi, mjini Iringa. Mng’ong’o ambaye pia alikuwa mmoja wa wenyeviti wa bunge la 10 linalomazima muda wake amekuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kwa miaka 15.