Skip to main content

Posts

Showing posts from April 20, 2017

Imebainika: Kumbe Marekani haikutuma meli za kivita Korea Kaskazini........Vilikuwa ni Vitisho Kwa Korea Kaskazini

Marekani na Korea Kaskazini zimeendelea kujibizana vikali, ambapo safari ya meli za kivita za Marekani ikiwemo meli yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita ya Carl Vinson imeibua hisia kubwa na uwezekano wa Marekani kufanya shambulio la mapema kujaribu kulemaza mfumo wa kijeshi wa Korea Kaskazini. Wakati taarifa hizo zikienea, imebainika kwamba meli hizo za kivita za Marekani hazikuwa zinaelekea upande wa Korea Kaskazini kama ilivyoripotiwa awali, bali zilikuwa zinaelekea eneo tofauti. Awali iliripotiwa kuwa, Jeshi la wanamaji la Marekani lilikuwa likielekea Korea kama hatua ya kuionya Korea Kaskazini, ambapo Rais Trump pia alitangaza kwamba kundi kubwa la meli za kivita lilikuwa likitumwa eneo hilo, hivyo imebainika kuwa si kweli. Hadi kufikia mwishoni mwa wiki, meli hizo zilikuwa zimesafiri mbali sana na rasi ya Korea na zilikuwa zinapitia mlango wa bahari wa Sunda kuingia katika Bahari ya Hindi. Wakuu wa jeshi la wanamaji la Marekani katika Bahari ya Pasi...

WATUMISHI WENYE VYETI FEKI SERIKALI WAFIKIA ELFU 10

Sakata la watumishi wa umma kushughi vyeti vya elimu limezidi kuchukua sura mpya na sasa wamefikia zaidi ya 10,000. Hatua hiyo, inatokana na uhakiki uliofanywa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo imebaini waombaji kazi 39,511 kati yao, 1,951 wana vyeti vya kughushi. Kuongezeka kwa idadi hiyo, kunatokana na kauli ya Rais Dk. John Magufuli, wiki iliyopita, kwamba anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali ambao wamebainika kuwa na vyeti feki. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam, wakati akizindua mabweni mapya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alisema anafahamu idadi ya watumishi wenye vyeti feki ni zaidi ya 9,000 na anaisubiri ripoti hiyo kuifanyia kazi. “Kwa hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo kwa sababu mlinichagua kwa ajili hiyo,” alisema Rais Magufuli....

POLISI DAR YAWATIA MBARONI WATU 267

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata watuhumiwa 267 kwa makosa mbalimbali ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha, utapeli, wizi, kucheza kamari, na kupatikana kwa dawa za kulevya, kuanzia Aprili 13 hadi 17,2017. Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 19, 2017 Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro amesema takribani kete 366 za dawa za kulevya, bhangi misokoto 51 na lita 200 za pombe haramu aina ya gongo zilikamatwa kufuatia operesheni kali iliyofanywa na askari polisi. “Pia Polisi wamekamata watuhumiwa watatu kwa wizi wa vitu mbalimbali maeneo ya Chamanzi wanaofahamika kwa majina ya Athuman Bashiru na Rashid Seleman na Mohamed Mussa. Pia wamekamata pikipiki moja ya wizi na kwamba watuhumiwa wawili wanashikiliwa kufuatia tukio hilo ambapo walimkata na panga kichwani mmiliki wake Ibrahim Shaban na kumpora pikipiki hiyo,” amesema. Aidha, amesema Jeshi la Polisi mnamo Aprili 10, 2017 limekamata watuhumiwa watano wa u...

20 DRIVERS TO PARTICIPATE IN IRINGA MOTOR RALLY

THE Chairperson of the Iringa Motor Sports Club (IMSC) Hamid Mbatta has urged citizens to take advantage of Iringa Motor rally to promote business due to the many visitors who come to the region to witness the event. He said that more than 500 guests and 20 drivers from within and outside the country are expecting to witness and participate in the race that will take place in Iringa at national level starting on 22-23 April this year. Mbatta said that racing is a great opportunity to do business with the promotion and strengthening of the tourism industry of the southern tourism circuit. He said that there are five ways selected for the competition in which more than 302 Km both (Completion section and the transport section) from the Mkwawa water factory located in Iringa who are major sponsors of the competition. He mentioned participants from Iringa known as Mkwawa Rally Team as Ahmed Huwel with his navigator Maisam Fazal who will be driving his new ca...

MADEREVA 20 KUSHIRIKI MASINDANO YA MAGARI MKOANI IRINGA

Mshiriki wa mashindano ya mbio za magari kutoka Iringa (Mkwawa Rally Team), Ahmed Huwel ambaye atatumia gari lake mpya aina ya Ford Fiesta akimkaribisha Dereva mkongwe wa mbio za magari nchini Gerald Miller (wa pili kulia) kutoka mkoani Arusha alipowasili jana, kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za magari yatakayofanyika kuanzia tarehe 22-23, mwezi Aprili mwaka huu mkoani Iringa. Mashindano hayo yanayoandaliwa na klabu ya mbio za magari ya Iringa (IMSC) kwa kushirikiana na kiwanda cha maji cha Mkwawa cha mjini Iringa. (Picha na Friday Simbaya ) Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wanahabari jana kuhusu Mashindano ya mbio za magari kitaifa yatakayoshirikisha madereva 20 wakiwa pamoja na wasaidizi wao kutoka ndani na nje ya nchi yanayoandaliwa na klabu ya mbio za magari ya Iringa (IMSC) kwa kushirikiana na kiwanda cha maji cha Mkwawa cha mjini Iringa. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa IMSC Hamid Mbatta na kushoto kwake ni Afande Steven Nyandongo wa...

MAKOTA FOREST YAKABIDHI BATI 20 NA MIFUKO YA CEMENT 100 KWA MKUU WA WILAYA KILOLO

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah (kushoto) akipokea msaada wa madawati 20 kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya Makota Forest Bharat Bhesania jana kampuni hiyo imetoa madawati hayo pamoja na bati 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu. KAMPUNI ya Makota Forest ya inayojihusisha na shughuli za Kilimo katika kata ya Ihimbo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imetoa msaada wa bati 100 pamoja na madawati 20 kwa ajili ya kuunga mkono serikali ya wilaya ya Kilolo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa . Akizungumza leo [jana] wakati wa kukabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah ,Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bharat Bhesania alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia shughuli mbali mbali za kimaendeleo katika wilaya ya Kilolo na maeneo mengine ya mkoa wa Iringa . Bhesania alisema kuwa jitihada zinazofanywa na viongozi wa wilaya ya Kilolo na mkoa wa Irin...