IRINGA WAANZA MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA Iringa. Katika juhudi za kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia (GBV), Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali umeanza kuandaa rasimu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, Watoto na Wanaume (MTAKUWA II) ngazi ya mkoa, kwa lengo la kuhakikisha ukatili unatokomezwa kwa kiwango cha juu kabisa. Kikao kazi cha maandalizi ya mpango huo wa kitaifa wa miaka mitano (MTAKUWA II 2024/25 – 2028/29), kiliongozwa jana na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Saida Mgeni, ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii mkoani humo. Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa MTAKUWA/NPA-VAWC mkoa wa Iringa, Grace Simalenga, alisema mpango mkakati wa awamu ya pili umejumuisha pia wanaume na wavulana ili kuhakikisha mapambano dhidi ya ukatili yanagusa makundi yote. “Leo tumekutana kupitia maandalizi ya mpango mkakati ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.