Skip to main content

Posts

Showing posts from September 17, 2015

UGEUGEU NA UPAPARA WA KUPATA FEDHA UNAKWAMISHA VIJANA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiingia katika ukumbi wa mkutano hoteli ya Double Tree by Hilton kwa ajili ya warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF. Na Mwandishi wetu VIJANA nchini Tanzania wanatakiwa kujitambua, kuacha kuwa kigeugeu na kufanya papara ya kupata fedha kama wanataka kuendelea na kufanikiwa kibinafsi na kiuchumi. Kauli hiyo imetolewea jana na Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga kwenye warsha ya wadau wa kitaifa ya kujadili suala la ajira kwa vijana Tanzania . Kauli yake hiyo kwa vijana hao waliojumuika katika hoteli ya DoubleTree by Hilton, Dar es salaam, ilitokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini ambazo zinaonesha kwamba vijana wengi hawana msimamo wa maisha, hawana maono, hawana malengo binafsi wala kutambua ma...

CCM WAPANIA KULIGOMBOA JIMBO LA IRINGA MJINI

Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga (Picha na Maktaba) KIU ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kukomboa Jimbo la Iringa Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, inazidi kuongezeka baada ya mgombea udiwani wa CCM kata ya kihesa kuwataka wananchi kutomchagua mbunge aliyemaliza muda wake kupitia chama cha demokrasia na maendelo (Chadema) Mch. Peter Msigwa kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake. Mgombea huyo wa ata ya Kihesa, Kenani Kihongosi Laban alitoa rai katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya Kihesa uliyofanyika viwanja vya kihesa sokoni jana. Alisema kuwa mbunge huyo anayemaliza muda wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) aliahidi kujenga soko la kisasa la kihesa lakini hadi miaka mitano inakwisha soko hilo halijajengwa. Aliomba wakazi wa kihesa wamchague katika uchaguzi mkuu wa 2015 iliakafanishe ujenzi wa soko hilo pamoja na mambo mengine ikiwemo masuala ya afya na elimu. Alisema kuwa watangulizi wak...