Skip to main content

Posts

Showing posts from April 30, 2017

DC KASESELA BANS CATCHING OF SMALL FISH AT MTERA DAM

By Friday Simbaya, Iringa IRINGA District Commissioner Richard Kasesela has banned exploitation of young fish that are below the maximum allowable three inches (3) because it is contributing to the destruction of fish hatcheries in Mtera Dam. He said that for a long time Mtera Dam has been facing the problem of illegal fishing using illegal fishing tools such as Kokoro, Gonga, and Kimia and Katuli type of fishing nets. Kasesela gave the directive yesterday during exercise destruction of 124 illegal fishing gears with fire held in the Migoli Village of Iringa district in Iringa region. He said that illegal fishing has resulted in reducing the rate of fish in Mtera Dam for fishing small sized fish under three inches (3) hence the destruction of fish hatcheries. "The presence of this dam has had benefits for the community, has enabled fisheries boost incomes and improve nutrition in the community since nearly 90 percent of the population of villages livin...

DC KASESELA APIGA MARUFUKU UVUAJI SAMAKI WACHANGA BWAWA LA MTERA

Na Friday Simbaya, Iringa, zana haramu za uvuvi za chomwa moto Migoli IRINGA: Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amepiga marufuku uvuaji wa samaki wachanga walio chini ya kiwango kinachoruhusiwa cha inchi tatu (3) kuankochangia uharibifu wa mazalia ya samaki katika Bwawa la Mtera.  Alisema kuwa kwa muda mrefu Bwawa la Mtera limekuwa likikabiliwa na tatizo la uvuvi haramu unaotumia zana haramu za uvuvi kama vile nyavu za kokoro, gonga, kimia na katuli.  Kasesela alitoa agizo hilo jana wakati wa zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi 124 kwa moto lililofanyika katika Kijiji cha Migoli, Taarafa ya Isimani wilayani Iringa, mkoani Iringa.  Alisema kuwa uvuvi haramu umepelekea kupunguza kiwango cha samaki katika Bwawa la Mtera kwa kuvua samaki wachanga walio chini ya inchi tatu (3) na kupelekea uharibifu wa mazalia ya samaki.  “Uwepo wa bwawa hili umekuwa na faida kwa jamii, umewezesha shughuli za uvuvi kuwaongezea kipato na ku...

IRINGA DC YATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA YA MAZINGIRA

Kikosi kazi cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha Mkuu kikikagua chanzo cha maji Kivalali kilichopo kijiji cha Bandabichi wilayani Iringa, mkoani Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya) Na Friday Simbaya, IRINGA Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imetakiwa kusimamia Sheria ya Mazingira vizuri ili kuondoa uharibifu wa mazingira katika bonde la mto Ruaha Mkuu. Agizo hilo lilitolewa na mwenyekiti wa kikosi kazi namba tatu cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha mkuu ambaye pia ni Katibu Tawala mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu wakati kikosi kazi hicho kilipokutana na timu ya menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa jana.  Ayubu alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Iringa inakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira. “Ndugu zangu, sheria ya Mazingira lazima isimamiwe ipasavyo. Katika kusimamia vizuri sheria hii wekeni utaratibu mzuri wa kusimamia sheria hii kwa kuziimarisha kamati za mazingira kuanzia ngazi za wilaya, kata na vijiji. Kamati hizi zikiimarishwa utekelezaj...