Na Friday Simbaya, Peramiho Timu ya wafanyakazi wa misioni ya Abasia Peramiho imeichapa Timu ya watumishi wa serikali mabao 4-2 Jumapili katika mashindano ya Mei Mosi 2011, yaliyofanyika katika viwanja vya Peramiho misioni, yakiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, wilayani Songea vijijini mkoani Ruvuma. Katika mechi hiyo kipindi cha kwanza timu zote mbili ziliaanza kwa kushambuliana, ambapo timu ya Peramiho Misioni walifanikwa kupata magoli mawili ya chapuchapu ambapo timu ya watumishi wa serikali hawakupata chochote hadi kipindi cha kwanza kimalizika. Kipindi cha pili kilipoanza timu ya watumishi iliaamka kutoka usingizini na kushumbulia lango la abasia ya Peramiho bila mafanikio na matokeo yake kuaacha mwanya kwa timu ya Abasia kuongeza magoli mengine mawili. Timu ya Abasia walibweteka na ushindi wa magoli manne na kuwadharau ndipo timu ya watumishi walicheza kufa na kupona na kurudisha magoli mawili dakika za mwisho na mpira kumaliza kwa matokeo 4-2...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.