Skip to main content

Posts

Showing posts from November 17, 2011

UHABA WA HUDUMA YA AFYA YAWAKUMBA WANANCHI WA KIJIJI CHA MLANGALI

Na Friday Simbaya, Ludewa Wananchi wa Kijiji cha Mlangali Kata ya Mlangali wilayani Ludewa, mkoani Iringa wameiomba serikali  iwafungulie zahanati yao waliyoijenga kwa nguvu zao wenyewe  ili waweze kupata huduma ya afya  jirani, kwa sasa wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta  matibabu katika Kituo  Cha Mlangali ambacho kipo zaidi ya kilometa nne. Wakiongea na Nipashe jana Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlangali Bw. David Mtitu na Mtendaji wa Kijiji  (VEO) Bw. Leo Mlelwa kwa pamoja walisema kuwa wananchi wa kijiji hicho wanapata shida sana kupata huduma ya afya kutokana na kijiji chao kukosa  zahanati, wakati wana zahanati yao waliyoijenga kwa nguvu zao. Walisema kuwa zahanati yao hipo tayari ,lakini hadi sasa haijafunguliwa. “Pamoja na kuitikia wito wa Serikali wa kutaka kila  kijiji kuwa na zahanati na sisi kama wanakijiji cha Mlangali tuliitikia wito huo na tukaamua kujenga zahanati yetu, lakini cha ...