Skip to main content

Posts

Showing posts from June 23, 2016

MAGAZETINI LEO IJUMAA

ASILIMIA 89 YA WATANZANIA WAMKUBALI RAIS MAGUFULI; UTAFITI WA CZI WABAINISHA

Mwanasheria msomi, kutoka taasisi huru inayojishughulisha na ushauri wa mambo ya habari, (CZI), David Saile Manoti, (katikati), akiwa na wasomi wenzake, Bi Dotto Nyirenda, (kushoto) na Juma George Chikawe, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Wanazuoni hao ambao ni wanachama wa CCM, wamesema utafiti unaonyesha Watanzania wengi wanaimani kubwa na Rais Magufuli katika mageuzi yake ya uchumi na nidhamu. David Saile Mnoti, Mwanasheria, czi NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID TAASISI ya ushauri wa mambo ya Habari ijulikanayo kama CZI, imetoa utafiti unaoonyesha kuwa katika kipindi cha miezi 8 ya utawala wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Watanzania wengiwanamkubali Rais na wanayo imani kubwa Tanzania itarudi kwenye “mstari’. Watafiti hao, ambao ni David Saile Manoti ambaye amebobea kwenye masuala ya Sheria, Juma George Chikawe, yeye ni mtaalamu wa Teknohama, na Dotto Nyirenda ambaye amebobea kwenye masuala ya Kidiplomasia, wame...

JPM AZINDUA SARAFU MPYA YA SHILINGI ELFU 50 WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BOT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua sarafu maalumu ya shilingi 50,000/- kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndullu, na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Khamisi Musa Omar Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango, Dkt Servacius Likwelile,(wapili kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedhana Mipango Zanzibar, Khamis Mussa Omar, (wakwanza kushoto), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, 9wapili kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Dar e3s salaam Mhe Paul Makonda(wakwanza kulia). kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph...