Skip to main content

Posts

Showing posts from September 20, 2016

Watanzania watakiwa kutunza mazingira

Na Rabi Hume, MO BLOG Kutokana na kuwepo na shughuli nyingi za kibinadamu ambazo zinaharibu mazingira, watanzania nchini kote wametakiwa kuwa makini kwa kutunza mazingira yanayowazunguka ili kuepusha matatizo ambayo yanaweza kutokea kutokana na kushindwa kudhibiti vitendo vya uharibifu mazingira. Rai hio imetolewa na Balozi Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Geneva, Uswisi, Modest Mero katika warsha ya kujadili kuhusu kilimo na biashara iliyoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF). Balozi Mero alisema kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa na shughuli nyingi ambazo zinaharibu mazingira hali ambayo inatishia maisha ya vizazi vijavyo na hivyo ni vyema watanzania wakaanza kuchukua hatua kwa kutunza mazingira ili kuepeusha athari ambazo zitajitokeza kwa miaka ijayo. "Dunia nzima watu wanakata miti, wanachoma majani mashambani lakini hawajui kama kuna vitu vya muhimu wanaua ardhini, na mimi niwambie watanzania wawe makini wasikate miti...