18:48 No comments MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imewahukumu kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Sh Milioni 1.5 kila mmoja, dereva Hansi Mwakyoma (28) na tingo wake wake Alex Adam (32) baada ya kukamatwa na kukiri kusafirisha wahamiaji wasio na vibali 83 kutoka nchini Ethiopia ambao pia wamehukumiwa kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya Sh Milioni 1. Kwa kutumia gari aina ya Scania lenye namba T478 DFE mali ya Frola Mwambenja wa Mbeya, Januari 16, mwaka huu; dereva huyo na tingo wake walikamatwa katika kijiji cha Ruaha Mbuyuni wilayani Kilolo mkoani Iringa, barabara kuu ya Iringa Mbeya wakiwasafirisha watu hao kuelekea Kyela ambako ni mpakani mwa Tanzania na Malawi. Akitoa hukumu hiyo leo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa Endrew Scout alisema ameridhika na maelezo yaliyotolea na wakili wa serikali pamoja na vielelezo likiwamo gari lililotumiwa na watuhumiwa hao kusafirisha watu hao kutoka Kongowe Dar es Salaam ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.