Meza kuu kwenye uzinduzi wa kambi ya upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo ya upimaji kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige, Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee, Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kibugumo, Mzamilo Ally, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog ). Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi nchini (Bango Sangho) umetoa msaada wa kompyuta, printa, tanki la maji la lita 5000, umeme, madarasa saba yaliyofanyiwa ukarabati, madaftari na kalamu katika Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni ulio na thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na huduma ya kupima ...