Skip to main content

Posts

Showing posts from February 28, 2026

Government Pays Tribute as Cardinal Pengo Is Laid to Rest

The Vice-President of the United Republic of Tanzania, Dr Emmanuel Nchimbi, represented President Dr Samia Suluhu Hassan at the funeral of retired Archbishop of the Archdiocese of Dar es Salaam, the late Polycarp Pengo. The funeral Mass was held at the Shrine of Our Lady of Lourdes – Pugu in Dar es Salaam, attended by religious leaders, government officials and members of the public who gathered to pay their last respects. Delivering the government’s condolence message after the Mass, Dr Nchimbi said the Government values Cardinal Pengo’s patriotism and his significant contribution to the nation’s spiritual and social development. He noted that the late Cardinal dedicated himself not only to Catholics but to all Tanzanians, regardless of their faith. He described Cardinal Pengo as a principled and upright leader who consistently emphasised the importance of living according to God’s commandments and respecting the laws of the country. According to the Vice-President, the values h...

Mazishi ya Kardinali Pengo: Serikali Yatambua Uzalendo na Mchango Wake kwa Taifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Marehemu Polycarp Pengo. Ibada ya mazishi imefanyika katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria – Pugu, jijini Dar es Salaam, ambapo waumini na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali walihudhuria kutoa heshima zao za mwisho. Akitoa salamu za rambirambi baada ya ibada, Dkt. Nchimbi amesema Serikali inathamini uzalendo na mchango mkubwa alioutoa Kardinali Pengo katika maendeleo ya nchi, kiroho na kimwili. Alisema marehemu alijitoa si kwa Wakatoliki pekee, bali kwa Watanzania wote bila kujali tofauti za imani. Ameeleza kuwa Kardinali Pengo alikuwa kiongozi mwadilifu aliyesisitiza kuishi maisha ya kufuata amri za Mungu na kuheshimu sheria za nchi. Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, maadili aliyoyafundisha na kuyaishi yanapaswa kuwa mwongozo kwa kila Mtanzania. Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa marehemu atakumb...

PRIME MINISTER ATTENDS FUNERAL OF CARDINAL PENGO IN DAR ES SALAAM

Prime Minister Dr Mwigulu Nchemba on February 28, 2026 attended the funeral of the retired Archbishop of the Catholic Archdiocese of Dar es Salaam, the late Polycarp Kardinali Pengo. The funeral service was held at the Church of the Pilgrimage of the Virgin Mary – Pugu in Dar es Salaam and was attended by hundreds of faithful, as well as national and religious leaders. The ceremony was led by the Vice-President of the United Republic of Tanzania, Emmanuel Nchimbi, who conveyed condolences on behalf of the Government and urged Tanzanians to honour Cardinal Pengo’s significant contribution to promoting moral values, peace and national unity. Other government officials, representatives of various institutions and leaders from different religious denominations also attended the service, describing the late Cardinal as a courageous and wise leader who served both the Church and the nation with integrity. The funeral service was led by Archbishop Ruwaichi Taddeus, who presided over the...

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZISHI YA KARDINALI PENGO DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Februari 28, 2026 ameshiriki mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. Ibada ya mazishi imefanyika katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria – Pugu, jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na mamia ya waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kidini. Mazishi hayo yameongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Emmanuel Nchimbi, ambaye alitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali na kuwataka Watanzania kuenzi mchango mkubwa wa Kardinali Pengo katika kulinda maadili, amani na mshikamano wa taifa. Viongozi wengine wa Serikali, wawakilishi wa taasisi mbalimbali pamoja na viongozi wa dini tofauti walihudhuria ibada hiyo, wakimtaja marehemu kama kiongozi jasiri na mwenye hekima aliyelitumikia Kanisa na Taifa kwa uadilifu mkubwa.  

Uchambuzi wa Kina wa Wimbo “Crazy World”

1. Dhamira Kuu: Unafiki na Maadili ya Jamii Katika wimbo huu, Lucky Dube anaeleza jinsi dunia ilivyojaa unafiki. Anaonyesha kuwa kuna watu wanaojifanya wema mbele ya hadhara, lakini mioyoni mwao hawana huruma wala uadilifu. Anakosoa tabia ya kuhukumu wengine wakati jamii yenyewe imejaa matatizo ya kimaadili. 2. Umasikini na Ukosefu wa Haki Mistari kama: “You can see them there on the street Begging for money…” Inaonesha hali halisi ya watu maskini wanaoishi mitaani. Msanii anauliza kimya kimya: Je, ni nani anayewajibika kwa hali hii? Anagusia pengo kati ya matajiri na maskini, na namna jamii inavyoweza kupuuza mateso ya wanyonge. 3. Dunia Iliyojaa Chuki na Migogoro Kwa kutumia kauli “Crazy World”, Lucky Dube anaielezea dunia kama sehemu isiyo na utulivu — yenye chuki, migawanyiko na ubinafsi. Hii inaendana na mazingira ya Afrika Kusini miaka ya 1990, kipindi ambacho taifa hilo lilikuwa linatoka katika mfumo wa ubaguzi wa rangi (apartheid). Muziki wake m...

Waombolezaji Wakwama Njiani Wakielekea Kwenye Mazishi

Iringa. Waombolezaji kutoka Manispaa ya Iringa wamejikuta wakikwama njiani kutokana na utelezi mkubwa uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha, walipokuwa wakielekea kuzika mpendwa wao, marehemu Mzee Vesdasto Myulla. Tukio hilo lilitokea katika barabara ya njiapanda ya Tosamaganga–Luhota, wilayani Iringa, ambapo magari yaliyokuwa yamebeba waombolezaji yalishindwa kupita kutokana na matope na utelezi mkali. Waombolezaji hao waliondoka mjini Iringa majira ya saa 8 mchana, baada ya ibada ya kuaga mwili iliyofanyika katika Mtaa wa Mwimbi B, Kata ya Makorogoni. Msafara huo ulikuwa ukielekea kwenye makaburi ya familia ya kina Myulla yaliyopo Luhota, Kata ya Ikuvilo, wilayani Iringa. Baadhi ya waombolezaji walilazimika kushuka kwenye magari na kusukuma ili kujaribu kuvuka eneo hilo, huku wengine wakilazimika kusubiri kwa muda hadi hali ya barabara iliporuhusu safari kuendelea. Wakizungumza kwa masikitiko, baadhi ya wananchi walisema changamoto ya barabara hiyo imekuwa ya muda mre...