Skip to main content

Posts

Showing posts from March 16, 2014

MAMIA YA WAKAZI WA PERAMIHO WAMZIKA BABA MZAZI WA RAIS WA VICOBA TANZANIA

Na Friday Simbaya, Songea Paroko Msaidizi wa Parokia ya Peramiho katika Jimbo Kuu la Songea, Padre Benedict OSB ametoa rai kwa wazazi wa Peramiho na kwingineko kuwaelekeza watoto katika masomo kwa sababu elimu ni mwanga wa maisha. Alisema kuwa wazazi na walezi wanapaswa kuwasomesha watoto wao ili kuwaandalia maisha mazuri kwa baadaye yenye faraja. Paroko huyu aliyasema haya jana wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya mazishi ya marehemu Barnabas Jacob Mkuwa (91), ambaye alikuwa baba mzazi wa Mbunge wa Viti Maalum, Rais wa Vicoba Tanzania na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Devote Mkuwa Likokola. Misa hiyo iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Madukani, Peramiho wilayani Songea, mkoani Ruvuma iliongozwa na mapadre saba, akiwemo Padre Lucius OSB aliyeongoza madhehebu yote ya Misa. Alisema kuwa kuna baadhi ya wazazi wanakwepa majukumu ya kuwalea watoto wao katika maadili mema ikiwa pamoja na kuwapatia elimu, afya, mavazi na malezi. “Watoto ni zawadi kwenu, simameni imara...