Skip to main content

Posts

Showing posts from November 19, 2015

Kampuni ya TTCL Yakisaidia Vifaa Tiba Kituo cha Afya Buguruni Dar

Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo. Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imetoa msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho. Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alve...

KASSIM MAJALIWA ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Na Khalfan Said RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli hatimaye ametungua kitendawili cha nani atakayekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kumteua Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi,  Kassim Majaliwa. Spika wa Bunge Job Ndugai, alipokea bahasha yenye jina la mteule huyo wa Rais, kutoka kwa Mpambe wa Rais, ambaye akiwa ndani ya sare zake za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, aliongozwa na wapambe wa Bunge hadi kwenye meza ya Spika Ndugai na kumkabidhi bahasha hiyo mapema  Novemba 19, 2015. Baada ya Mh. Ndugai kupokea bahasha hiyo aliwaonyesha wabunge na kusema bahasha hii imewekewa seal, hivyo akamwita Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila na kumtaka aifungue ili kujua jina la Waziri Mkuu ni nani. Dkt. Kashilila aliifungua bahasha hiyo na kukumbana na bahasha ya pili, hata alipoifungua bahasha hiyo ya pili akakumbana na bahasha ya tatu na ilipofungunliwa akakutana na kadi maalum yenye ujumbe ul...

MWANAHABARI NASHON KENEDY AWAPA SIRI YA MAFANIKIO WAIGIZAJI WA FILAMU JIJINI MWANZA

Kulia ni Mwanahabari Nashon Kenedy kutoka gazeti la kiswahili la Habari Leo na lile la kiingereza la Daily News akiongea katika hafla ya kuzaliwa kwa Yusuph Kisiba a.k.a Yuskiss ambae ni Mtengenezaji wa Filamu katika Kampuni ya Shafineyz Film Production ya Jijini Mwanza. Na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group Mwanahabari Nashon Kenedy kutoka gazeti la kiswahili la Habari Leo na lile la kiingereza la Daily News amewashauri wasanii wa maigizo Jijini Mwanza, kubadilika na kuigiza filamu zinazogusa maisha halisi ya Kitanzania na kuachana na uigizaji wa filamu zisizo na uhalisia wa maisha ya Kitanzania hususani filamu za mapenzi.  Kenedy aliyasema hayo jana katika hafla ya kuzaliwa kwa Yusuph Kisiba a.k.a Yuskiss ambae ni Mtengenezaji wa Filamu katika Kampuni ya Shafineyz Film Production ya Jijini Mwanza ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo pamoja na wageni wengine, pia ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu kutoka Jijini Mwanz...

UN WAZINDUA MRADI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akipanda mti kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs). Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimwagilia maji kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino...

VITABU HIVYO VINAPATIKANA...

Mtunzi; ELIAS K. MWALONGO(KANTON) Mahali; PERAMIHO MAJOR SEMINARY Mawasiliano; P.O.Box 977, Njombe VITABU HIVYO VINAPATIKANA; .NDANDA BOOKSHOP MTWARA .TMP BOOKSHOP TABORA .PERAMIHO BOOKSHOP .SONGEA BOOKSHOP .PERAMIHO MAJOR SEMINARY AU PIGA SIMU 0769313224 UPATE MAELEKEZO. ASANTE SANA

MAGAZETINI LEO IJUMAA NA SIMBAYABLOG

M

'Matumizi ya choo na unawaji wa mikono kwa sabuni bado vikiwa bado vipo chini'

IRINGA: JUMLA ya kaya 201,120 ambayo ni sawa na asilimia 89 mkoani Iringa zina vyoo na kati ya Kaya hizo asilimia 17 tu ndiyo zenye vyoo bora.  Kauli hiyo imetolewa jana na katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo ya kuhamamisisha wanahabari juu ya usafi wa mazingira. Ayubu alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwa kuwajengea uwezo wanahabari kujua mambo muhimu yanayohusiana usafi wa mazingira na matumizi ya choo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira hapa nchini. Alisema kuwa hali ya unawaji mikono kwa sabuni ni sawa na asilimia tisa huku hali ya matumizi ya choo na unawaji wa mikono kwa sabuni bado vikiwa bado vipo chini. Naye ofisa afya wa mkoa wa Iringa Khadija Haroun alisema mafunzo hayo yanaenda sambamba na wiki ya usafi wa mazingira hapa nchini. Haroun alisema kuwa watu takriban milioni 1.8 wanakufa kila mwaka duniani kote kutokana na magonjwa ya kuhara. Alisema kuwa watoto chini ya miaka mitano ...

'Awareness on use of soap to wash hands still very low'

BY FRIDAY SIMBAYA As the country celebrates climax of the national sanitation week today in Njombe Region, the public is reminded that use of soap to wash hands remains very low as does the availability of improved toilet facilities. The National Sanitation Week combines Global Hand-Washing Day and World Toilet day and has been observed as of November 15 –19. Speaking during the official opening of a capacity training for journalists on covering sanitation matters, the Regional Administrative Secretary (RAS), Wamoja Ayubu said a total of 201, 120 households (89 per cent) have toilets in Iringa but only 17 percent have improved toilets. “Hand washing with soap is only at nine percent,” she decried. On her part, Khadija Haroun a health officer for Iringa said about 1.8 million people die every year worldwide due to diarrhea and 760,000 children under five years of age die every year from diarrhea related diseases. “In Tanzania, about 30,000 people die each yea...