Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasilisha mtazamo wa namna ambavyo anataka Wilaya hiyo iwe. Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji. Mathias Canal, Singida Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi Mkoani Singida hii leo wamepatiwa mafunzo ya kutambua mipaka ya majukumu yao kiutendaji katika kikao cha kazi kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ikungi. Mafunzo hayo yameandaliwa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kutokana na kubainika kuwa asilimia kubwa ya watendaji hususani wenyeviti wa vijiji na vitongoji wamekuwa wakiingilia katika majukumu ya kiutendaji.
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.