Kulia ni Bi.Vileth Muhamusi ambae ni mmoja wa Wajasiriamali Jijini Mwanza akizungumza na Mwandishi wa taarifa hii, George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group (BMG). Wanawake Mkoani Mwanza wametakiwa kutobweteka na kukaa majumbani bila kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali, kwa kuwa hatua hiyo inawafanya kuwa tegemezi katika jamii. Bi.Vileth Muhamusi ambae ni mmoja wa w ajasiriamali maarufu Jijini Mwanza, anaejishughulisha na biashara ya bustani hususan kuotesha miche mbalimbali ikiwemo miche ya mbao, matunda pamoja na kimvuli, aliyasema hayo jana wakati akizungumzia tatizo la ukosefu wa ajira kwa akina mama ambalo hivi sasa limegeuka janga kwa malezi ya watoto kutokana na baadhi yao kuwatumia watoto wao katika shughuli za kuomba omba mitaani ili kupata fedha za kujikimu kimaisha. Bi.Muhamusi anaepatikana katika bustani zilizopo pembezoni mwa Ziwa Victoria katika barabara ya Makongoro Jijini Mwanza, ali...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.