HALMASHAURI ya Wilaya ya Mufindi itatumia jumla ya shilingi Milioni Mia nne (400) kujenga na kufanya ukarabati mkubwa wa kituo cha Afya Malangali, kilichopo kata ya Malangali Halmashauri ya Wilayani Mufindi, ikiwa ni mkakati wa Serikali kuimarisha sekta muhimu ya Afya hususani Afya ya Mama na Mtoto. Profesa Riziki Shemdoe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi alisema ujenzi na ukarabati wa kituo hiki cha Afya, unaotarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa, unafanyika baada ya Ofisi ya Rais – Tamisemi, kutoa kiasi cha Shilingi Milioni mianne (400) kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya kituo hicho ili kiweze kukidhi haja ya kutoa huduma bora za Afya kwa zaidi ya Wananchi elfu arobaini na nane (48,000) wa Tarafa ya Malangali watakao pewa rufaa kutoka kwenye Zahanati za Vijiji. Alisema matumizi ya kiasi hicho cha fedha, ni pamoja na kujenga jengo la kisasa la Maabara, Nyumba ya Mganga, kukamilisha ujenzi unaoendelea wa chumba cha upasuaji sanjari ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.