Skip to main content

Posts

Showing posts from March 27, 2016

Binadamu amejipaka uchafu: Askofu Ngalalekumtwa

BINADAMU anaelezwa kuwa ni kiumbe kilichochafuka na uchafu wa kutisha ambao anahitaji msaada kwa ajili ya kusafishwa. Haya yamezungumzwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alipokuwa akihubiri katika Mkesha wa Pasaka Parokia ya Bikira Maria Consolata - Mshindo Jimbo la Iringa. Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa jimbo la Iringa alisema binadamu amejaa maovu ya kila aina ambayo yamekuwa kikwazo kwa wengine na kusema kuwa bila nguvu ya Mungu mwanadamu pekee hayawezi. "Kristo amekuja kututoa katika uhuni, ufisadi, unyang'anyi na dhuruma. Maovu yetu tuliyo nayo yanatokana na ukaidi wetu na kiburi. Amebeba dhambi zetu akafa msalabani kwa ajili ya kutukomboa utumwani mwa shetani. "Tumejipaka mavi, mikojo na uchafu wa kila aina. Tumejaa uchafu hata tumekuwa kinyaa, hatutamaniki kwa wengine. Sasa tumekombolewa kwa damu ya mwana kondoo" amesema. Amesema mwanadamu ameingia mkataba wa urafiki na i...