Skip to main content

Posts

Showing posts from July 3, 2015

CCM: TUTAKATA RUFAA KESI ZA MADAI ZILIZOTUPWA NA MAHAKAMA

Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini wanatarajia kukata rufaa kupinga kuondolewa kwa kesi nane za madai zilizotupiliwa mbali na mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya iringa, ili ziwezekusikilizwa tena baada ya Chadema kupeleka pingamizi zao mahakamani. Chama hicho kinachowakilishwa na wakili msomi, Gaster Likatage Mdegela kiliongea na Nipashe jana kuwa wako mbioni kukata rufaa kwa zile kesi za madai zilizoondolewa mahakamani awali kwa vigezo kuwa zilikosa mashiko. 

CHUO KIKUU CHA IRINGA KESHO KINATARAJIA KUADHIMISHA SIKU YA UTALII NA UTAMADUNI

MHADHILI WA CHUO KIKUU  CHA IRINGA JIMSON SANGA  baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani tumaini baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani tumaini na fredy mgunda,iringa Chuo kikuu cha IRINGA ZAMANI TUMAINI kesho kinatarajiwa kuadhimisha siku ya utalii wa kitamaduni katika chuo hicho. Akizungumza na blog hii mkuu wa kitengo cha utalii cha chuo hicho MHADHILI WA CHUO KIKUU  CHA IRINGA JIMSON SANGA amesema kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo ili  kuwakumbusha wananchi juu ya kuuezi utamaduni wao na kuacha kuiga tamaduni za  kigeni. Aidha SANGA amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikifundisha elimu ya utalii ndani ya chuo tu sasa imefika wakati wa kutoka na kuifikia moja  kwa moja jamii ambayo haina elimu hiyo. “Tunaona wakina mama ntilie wanauza vyakula ya kitamaduni lakini hawana wateja kwa sababu wanashindwa kutoa huduma ya kuridhisha kwa  wateja hata hivyo mama ntilie wengin...