Skip to main content

Posts

Showing posts from January 13, 2018

DC ALI HAPI AZIPONGEZA DAWASA NA DAWASCO KWA USIMAMIZI MZURI ...

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe., Ali Hapi, (katikati), akiteremka kutoka juu ya tenki kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji wilayani kwake Januari 13, 2018. MKUU wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji wilayani kwake kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo kama ambavyo mkataba unaelekeza. Mhe. Hapi aliyasema hayo leo Januari 13, 2018 mwishoni mwa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundomnbinu hiyo inayohusisha matenki makubwa manne na vituo vinne vya kusukuma maji (Booster Stations) ikiwa ni pamoja na utandikaji wa mabomba ya kusafirisha maji. Mradi huo ambao unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (DAWASA), ni sehemu ya mradi mkubwa wa ubores...