Skip to main content

Posts

Showing posts from July 19, 2015

CCM WILAYA YA IRINGA MJINI YAANZA KUWATAMBULISHA WAGOMBEA UBUNGE KWA WANACHAMA

Katibu wa Wilaya ya Iringa mjini, Elisha Mwampashi (kulia) akiongea na waandishi wa habari jioni leo na kushoto ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Iringa mjini Abeid Kiponza. Zoezi la awali la utoaji na urejeshaji wa fomu kwa wagombea nafasi za ubunge na madiwani kupitia Chama cha Mapidunzi (CCM) nchi nzima umekamilika jana. Katika Jimbo la Iringa mjini, mkoani Iringa chama hicho kimeandaa mikutano kwa wagombea ubunge wote ya kuwatambulisha kwa wanachama ikiwa sehemu ya pili ya mchakato ya kumpata mgombea pekee atakaye peperusha bendera ya chama hicho kwa kushindana na vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana usiku, Katibu wa Wilaya ya Iringa mjini, Elisha Mwampashi alisema awamu ya kwanza ya kutoa na kurudisha fomu za ubunge limealianza tarehe 15.07.2015 na kumalizika hadi 19.07.2015. Aliongeza kuwa awamu ya pili ya mchakato itaanza tarehe 20.07.2015 hadi 31.07.2015 lengo ni kuwatambulisha watia nia kwa wa...

MCHUNGAJI MSIGWA APATA MAPOKEZI MAKUBWA IRINGA..!

Sehemu ya umati wa wakazi wa Iringa mjini wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa leo. (Picha na Friday Simbaya) Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu wakihutubia wa wakazi wa Iringa mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa katika Jimbo la Iringa mjini leo. (Picha na Friday Simbaya)